Monday, February 28, 2011

NDOA INATAKA KUNISHINDA JAMANI- NIFANYAJE NIINUSURU?


Mimi ni mama wa mtoto 1 nina miezi 6 tangu nimefunga ndoa, pia nina umri wa miaka 24. Tatizo langu ni kwamba simuelewi mume wangu kama kweli ananipenda au alinioa tu kwa sababu nilimzalia mtoto? Kwa sasa mi ni mama wa nyumbani nimemaliza chuo kikuu mwaka jana na mpaka sasa sijabahatika kupata ajira.

Kwanza mume wangu alianza kuwa ananifokea hovyo hata mbele ya wageni kwa makosa madogomadogo. Pia ni mwezi wa 3 sasa  mume wangu amekuwa na desturi ya kurudi usiku wa manane  akiwa amelewa au hata alfajiri siku nyingine na mara nyingi siku za weekend huwa harudi nyumbani. kwa kweli huwa naumia sana na mara nyingi huwa nalia na kusali peke yangu maana nikijaribu kuongea nae kumuuliza nini tatizo mbona unanifanyia hivi huwa ananijibu "unataka nisirudi kabisa au?" Naona aibu kuwaambia wazazi kuhusu hili maana ni muda mfupi sana tangu tumefunga ndoa.

Kuna kipindi nirijaribu kumshirikisha bestfriend wake labda kama angeweza kunisaidia kwa kumshauri rafiki yake ila cha kusikitisha nayeye  akanitaka kimapenzi. Yaani sielewi maana somatimes nahisi labda mume wangu kalogwa

. Ila cha kushangaza ni kwamba mume wangu ana wivu sana na mimi kila mara anakagua simu yangu, hataki niende hata saluni kanisani kwenyewe naenda kwa kulazimisha ila huwa naona kama hafurahii. Sikumbuki mara ya mwisho mume wangu kwenda ni lini.

Kuna kipindi nilijaribu kuangalia simu yake kwa kweli niliumia sana kwani nilikuta kanisave 'mama com' na si 'wife' kama alivyokuwa amenisave mwanzoni.
 
Kwa kweli watanzania naombeni ushauri wenu maana naogopa naweza kuja kuambukizwa gonjwa la Ukimwi kwani mimi bado ni mdogo na bado nina ndoto zangu nyingi.

Nampenda sana mume wangu  ila simuelewi kwa kweli. tumeishi miaka 3 kabla ya kufunga nae ndoa na hakuwa hivi alinipenda sana hadi watu na rafiki zangu hawakusita kuniambia jinsi alivyokuwa ananipenda. Natamani angeniambia nilichomkosea mume wangu kwani ninajaribu sana kuwa good wife but he never appreciate it. 

Tafadhali naombeni ushari wenu  watanzania wenzangu.

NIMERUDI RASMI WAPENZI WANGU-POLENI KWA KUWATUPA MUDA MREFU

nimerudi wapenzi wangu, baada ya kukimbia kama mwezi mmoja haivi, kutokana na mitihani iliyokuwa mbele yangu, but thanks God, coz nimemaliza mitihani, japo kabla ya kumaliza, tukakumbwa na mabomu, basi lo! mshike mshike kwenda mbele yani, ila namshukuru Mungu kwakuwa mimi na familia yangu tulinusurika, japo zile mbio nilizokimbia zilinifanya nipelekwe hospitali, 
im back dears, niliwamiss sana, pia mliotuma mikasa yenu, msijali, nitairusha hewani na kila kitu kitakwenda fresh kabisa, naanza na wale wa mwanzo na kuendelea, 
nawapenda

Tuesday, February 8, 2011

POLENI KWA UKIMYA WANGU DEARS

wapendwa wangu, niliwatupa kwa muda, kulikuwa na tatizo la kiufundi kidogo kwenye blog yangu hali iliyopelekea kuuchuna kulikopilitilza, bu now mambo shwari kabisa, mliotuma mikasa yenu niliiweka kapuni na tutaanza kuifanyia kazi soon.
na pia nawaaga jamani, naanza likizo kwa ajili ya mitihani ya kumaliza mwaka wa kwanza, so nitakuwa busy sanaaa na kitabu kwa kipindi hiki after that mambo yatakwenda kama yalivyopangwa, niliwamis na nawapenda sanaaaaa.